Languages
Content Who? About us Events Submissions Submenu
« back

Nisamehe

Jùmọké Bọlanle Adéyanju (2018)

Nimesahau rangi ya ukoloni

na mfuko ya maafa sokoni

nisamehe.

 

Walibadilisha jina lako

kutawala shina lako

nisamehe.

 

Damu ya upotevu katika mshipa wangu

umesikia maumivu yangu

nisamehe.

 

Bado hatujapata uhuru

kuwa mweusi leo ni vurugu

nisamehe.

 

Dawa ya kufanya leo iko sawa

sina, wallahi

wametuleta madharau

lakini

 

ukiendesha hewani

mwambie shetani

inatosha jamani!

 

Ubinadamu hamna

damu yetu yameibiwa

yani tangu umezaliwa

laana.

nahofu tu

kufa kupona.

 

Usisahau rangi ya ukoloni

na mfuko ya maafa sokoni

na kuishi

kuishi

 

kuishi.

© Jumoke Adeyanju

≡ Menu ≡
Homepage Content
Events Submissions
Authors Translators Moderators
About us Partners Gallery
Contact Blog Facebook
Festival 2016 Events Press